Consumer help Desk
Watumiaji wa huduma za nishati na maji zinazodhibitiwa na EWURA wanao wigo mpana wa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya huduma wanazozitumia kwa kufuata utaratibu ufuata:-
1. Kuandika barua na kuwasilisha kwa Mtoa Huduma na kubaki na nakala moja
2. Kujaza fomu ya malalamiko ya EWURA kama mlalamikaji atakuwa hajaridhika na namna lalamiko lake lilivyoshughulikiwa
3. Kukata rufaa kwenda Baraza la Ushindani (FCT) akipinga maamuzi/Hukumu iliyotolewa na Mdhibiti
Malalamiko yanayoweza kulalamikiwa ni pamoja na kuunguliwa vitu ama nyumba kulikosababishwa na majanga ya moto wa umeme, kucheleweshewa huduma baada ya kulipia, kukatiwa huduma kimakosa, bili kubwa zisizoendana na matumizi halali, umeme mdogo nk
Muhimu: Zingatia muda wa kuwasilisha malalamiko yako kama ulivyoainishwa kwenye Kanuni za kuwasilisha na kushughulikia malalamiko za EWURA (2013) ili upate haki yako!