Council Members
Chairman
Prof. Epaphrah Mushi
E.K Mushi ni mwalimu wa chuo kikuu (mstaafu), amebobea katika taaluma ya ukufunzi. Alianza kuhudumu katika nafasi ya Mkufunzi Msaidizi mwaka 1974 hadi kufikia kuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) katika Taasisi ya zamani ya Chuo cha Maendeleo (Institue of Development Management) na sasa Chuo Kikuu Mzumbe. Mushi amekuwa akifanya tafiti na kutoa ushari wa kitaalamu kwa ngazi za kitaifa na kimataifa katika fani za Mpango-miradi, Usimamizi na Ufuatiliaji pamoja na Tathmini. Katika utumishi wake, Mushi amepata kuteuliwa na kuhudumu kama Mkuu wa Idara kadhaa ikiwemo Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu Mzumbe. Alikuwa Meneja wa Mradi wa Usafiri, Meneja wa Mradi wa Ukarabati uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) na Meneja wa Hoteli ya Lumumba Complex katika Chuo Kikuu cha Mzumbe. Pia amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji ya mkoa ya EWURA CCC mkoa wa Morogoro (Morogoro RCC) kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji Oktoba 2017, nafasi anayoitumikia hadi sasa.